Magofu, viwanja vyatumika kutupia taka Bububu Kigamboni
13 September 2024, 3:45 pm
Na Mulkhat Mrisho Bushir,
Mwananchi wa shehia ya Bububu Kigamboni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja amelalamikia vitendo vya baadhi ya wananchi wanaotupa taka hovyo katika maeneo yasiyo rasmi hususani kwenye kiwanja vilivyo wazi na magofu ya nyumba ambazo hazijaisha.
Akizungumza na Zenji FM Bububu Kigamboni amesema kuna baadhi ya wananchi wanaotupa takataka katika eneo hilo la kiwanja ambacho kipo karibu na nyumba yake jambo ambalo linahatarisha usalama wa wakazi wa eneo hilo.
Aidha mwananchi huyo ameiomba serikali kupitia uongozi wa shehia kumtafuta mwenye kiwanja hicho ili kutatua changamoto ya utupwaji wa taka katika eneo hilo.
Naye sheha wa shehia Bububu Kigamboni Halima Twaha amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuwataka wananchi wenye tabia hyo kuacha mara moja kwani serikali haitasita kuwachukulia hatua kali kila mwananchi atakayejihusisha na utupaji taka katika kiwanja hicho.