Zenj FM

Elimu ya msaada wa kisheria kuwafikia wananchi Wilaya ya Kati

11 September 2024, 5:12 pm

Mwenyekiti wa Kamati ya Msaada wa KiSheria Baraza la Mji Kati Mussa Haji Mussa, akiwa na Mkuu wa Divisheni ya Uratibu wa Masuala ya Katiba na Msaada wa Kisheria Moza Rajabu Baraka kushoto ni Katibu wa Kamati ya Msaada wa Kisaheria Wilaya ya Kati Sabra Farouk Tahir wakiwa katika kikao cha pili cha kujadili mpango kazi wa Msaada wa Kisheria.

Na Mary Julius

Mwenyekiti wa Kamati ya Msaada wa Kisheria Baraza la Mji Kati Mussa Haji Mussa, amesema kutokana na uelewa mdogo wa sheria zilizopo nchini kamati hiyo imeamua kushuka kwa wananchi  ili kuwajengea uelewa wa sheria.

Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Baraza la Mji Kati uliopo Dunga,  katika kikao cha pili cha kujadili mpango kazi wa Msaada wa Kisheria,  kwa lengo la kuwajengea uwelewa wa mambo mbalimbali yanayo husiana  na Sheria pamoja na kupata msaada wa haraka wakati wanapofikwa na matatizo ya kisheria.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kamati ya Msaada wa Kisheria Baraza la Mji Kati Mussa Haji Mussa,

Mkuu wa Divisheni ya Uratibu wa maswala ya Katiba,  kutoka Idara ya Katiba na msaada wa kisheria Moza Rajab Baraka,  amesema Baraza la Mji Kati limekua ni chachu kwa Mabaraza mengine ya Mji, katika kuhakikisha elimu ya utoaji wa Msaada wa Kisheria kwa wananchi inafikiwa, katika Shehia tofauti ambazo zimo ndani ya Mabaraza hayo.

Sauti ya Mkuu wa Divisheni ya Uratibu wa maswala ya Katiba,  kutoka Idara ya Katiba na msaada wa kisheria Moza Rajab Baraka,

 Kwa upande wake Sabra Farouk Tahir ambaye ni Katibu wa Kamati ya Msaada wa Kisheria Wilaya ya Kati,  ameyataja baadhi ya maeneo yaliyojumuisha Wadi na Shehia za Wilaya ya Kati ambazo tayari wameanza kuzifanyia kazi kwa kutoa elimu hiyo ikiwa ni pamoja na Shehia ya Mchangani,  Hanyegwa mchana,  Tunguu,  Dimani, Marumbi, Kidimni na Shehia ya Bungi.

Sauti ya Katibu wa Kamati ya Msaada wa Kisheria Wilaya ya Kati Sabra Farouk Tahir.

Nae Sheha wa Shehia ya Binguni Ali Yussuf Mussa ambae pia ni Mwenyekiti wa Masheha wa Wilaya ya Kati Unguja,amewataka wajumbe kufikisha elimu ya Msaada wa Kisheria kwa wananchi ili lengo la Serikali la kuhakikisha vitendo vya udhalilishaji vinapungua liweze kufikiwa.

Sauti ya Sheha wa Shehia ya Binguni Ali Yussuf Mussa.