Sababu ACT Wazalendo kuunda baraza la mawaziri kivuli Zanzibar
7 September 2024, 12:08 am
Na Mary Julius.
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman, amesema baraza hilo ni fursa na jukwaa muhimu la kuwawezesha wananchi kusimamiwa maslahi yao kwa ukaribu zaidi na fursa ya kuweza kuyasimamia vyema maeneo yote yaliyoainisha kwenye sekta hizo.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo taifa Othman Masoud Othman, ametangaza rasmi Baraza kivuli la Mawaziri litakalosimamia utendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lenye Wasemaji wa Kisekta katika jumla ya maeneo 16 ambapo litafanyakazi kwa upande wa Zanzibar.
Othman ametangaza Baraza hilo katika mkutano maalum na vyombo vya habari huko katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembe Samaki mjini Zanzibar baada ya kuagizwa na Kiongozi wa Chama hicho ndugu Doroth Semu.
Amesema hatua ya kuundwa kwa Baraza hilo inatokana na Katiba ya Zanzibar kifungu cha tisa mabano mbili (a) kinachotamka kwamba Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatokana na wananchi wenyewe.
Othman amesema muundo wa Baraza hilo umezingatia sekta zilizopo Zanzibar bila kujali majina ya muundo wa wizara za Zanzibar , lakini limezingatia zaidi mtanzamo wa ACT –Wazalendo juu ya usimamizi wa sekta hizo kwa ufanisi.
Amesema baraza hilo litaongozwa na Mkuu na Kiongozi wa Baraza ambapo chini ya ofisi yake atakuwepo msemaji wa kisekta akisaidiwa na Naibu wake sambamba na Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza atakayekuwa chini ya Ofisi hiyo.
Aidha amesema kwamba hilo baraza hilo litafutalia mambo mbali mbali kwa kuzingatia maslahi ya wananchi hasa katika matumizi ya madaraka , rasilimali na fursa za nchi kuona kwamba malengo yaliyoelezwa ndani ya Katiba ya Zanzibar naya ACT- Wazalendo yanatimizwa kwa ukamilifu.
Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Ismail Jusa ameelezea mkakati wa baraza hilo kivuli la chama cha ACT wazalendo ambapo amesema baraza hilo litakuwa sehemu ya kuwasemea wananchi pamoja na kuibua na ufisadi uliopo serikalini.
Nao mawaziri walio teuliwa wamesema watahakikisha wanaongali kero za wananchi na kuzimesema pamoja na kuangalia utekelezaji wa ahadi za Chama Cha Mapinduzi.