Zenj FM

Wafugaji kuku wa kisasa Zanzibar watakiwa kulinda afya za walaji

6 September 2024, 6:44 pm

Picha ya kuku wa kisasa bandani.

Na Khalida Abdulrahman.

Kutokana na ongezeko kubwa la watumiaji wa kuku wa kisasa aina ya (broiler) wafugaji wametakiwa waache kuwapa dawa ovyo kuku hao ili kupunguza madhara kwa binaadamu.

  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mifugo Asha Zahran Mohammed ameyasema hayo huko Maruhubi Wilaya Mjini Mkoa Wa Mjini Magharibi Unguja.

Amesema wafugaji wa kuku wanatakiwa kufuata maelekezo ya daktari wa mifugo ili kupunguza athari kwa binaadamu ikiwemo vimelea sugu mwilini.

 Kwa upande wake Daktari wa Mifugo Fatma Ali amesema  mtumiaji wa  kuku broila anaweza kupata shida ya  usugu wa vimelea dhidi ya dawa mwilini pia husababisha mtumiaji kua na mafuta mengi mwilini  kutokana na vyakula wanavyopewa kuku hao.

Aidha  ametoa ushauri kwa wafugaji kutumia dawa kwa kufuata ushauri wa daktari ili kuwakinga walaji wa kuku na maradhi.

Sauti ya Daktari wa Mifugo Fatma Ali.