Wakazi wa shehia ya Sharifu Hamsi walia na wizi wa mifugo, mazao
6 September 2024, 6:25 pm
Na Jessca Pendael
Wakazi wa shehia ya Sharifu Hamsi Bububu wamesema kumekuwa ongezeko la wizi wa kuku, mbuzi na madafu katika shehia yao hali ambayo unarudisha nyuma maendeleo ya wakazi hao.
Wakizungumza na Zenji fm wakazi wa shehiaya hiyo wamesema wizi huo umekuwa kero katika eneo hilo hasa wizi wa madafu na mbuzi jambo ambalo limekuwa likichangia kurudisha nyuma juhudi za kujikomboa katika umaskini kwa wakazi waeneo hilo
wamesema katika shehia hiyo kipindi cha nyuma kulikuwepo na wizi wa kukaba kwa kutumia silaha kali lakini jeshi la polisi kwa kushirikiana na polis jamii waliweza walifanikiwa kumkamata mwizi mmoja na kumchukulia hatua za kisheria.
Aidha wamewaomba wakazi wa shehia hiyo kushirikiana ili kutokomeza wizi wa huo ulio ibuka hivi karibuni na kuomba adhabu kali kwa atakaye kamatwa ili kukomesha tabia hiyo ya wizi.
Kwa upande wake Sheha wa Shehiya ya Sharifu Hamsi wanu Makame Hassan amekiri kuwapo kwa wizi katika shehiya yake ambapo amesema wizi umesababishwa na baadhi ya wakazi wa shehia hiyo kutokuwa makini na mali zao hivyo anawasa wanajamii kuwa makini na mali zao ili kuepusha na kupata hasara.