Zenj FM

Asma Mwinyi aguswa na tukio la watoto watatu kuungua moto wilaya ya Magharib B

2 September 2024, 4:03 pm

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Asma Mwinyi Foundation Asma Ali Mwinyi akiwa na mama mzazi wa watoto walio ungua moto Warda Issa Said.

Na Mary Julius

Kufuatia tukio la kuungua nyumba na kusababisha kuungua watoto watatu wa Familia moja Taasisi ya Asma Mwinyi Fondation imefika katika nyumba iliyopata maafa hayo pamoja na kuwakagua watoto hao Hospitali walipolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Akizungumza mara baada ya kufika kuifariji Familia hiyo huko Katika Hospitali ya Wilaya Ijitimai Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Asma Mwinyi Foundation Asma Ali Mwinyi amesema athari iliyopatikana ni kubwa hivyo

Taasisi hiyo imeguswa na tukio hilo na kufika kutoa pole kwa athari waliyoipata.

Amesema kutokana na kuguswa na tukio hilo taasisi ya Asma Mwinyi imeona kuna umuhimu wa kuitembelea familia hiyo ili kuweza kuifariji katika kipindi hiki kigumu pamoja na kuwasaidia kutokana na athari iliyojitokeza.

Sauti ya Mkurugenzi wa Asma Mwinyi Foundation Asma Ali Mwinyi.

Msimamizi wa Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai Leonad Godini Mgana amesema wamewapatia matibabu watoto hao kutokana athari kubwa walioipata kuungua haswa katika sehemu za uso na wanatarajia kuwapa rufaa ya Mnazi mmoja ili kwenda kuendelea na matibabu.

Sauti ya Msimamizi wa Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai Leonad Godini Mgana.

Mama Mzazi wa Watoto hao Warda Issa Said na baba mzazi Issa Abdalla wameishukuru taasisi ya Asma Mwinyi Fondation kwa kuja kuwafariji kutokana na athari waliyoipata.

Sauti ya Mzazi wa Watoto hao Warda Issa Said na baba mzazi Issa Abdalla.

Tukio hilo la Moto liliosababishwa na kuanguka mshumaa katika chumba walichokuwa wamelala watoto hao limesababisha athari Mbali mbali ikiwemo kuungua watoto pamoja na kuungua baadhi ya vifaa katika nyumba hiyo.