Waislam watakiwa kutoa kipaumbele uhifadhi Quran kwa watoto
19 August 2024, 6:02 pm
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Alhaj Ayoub Mohd Mahmoud (aliyevaa kanzu nyeupe) akiwa na Wajumbe wa kamati Kuu ya Jumuiya ya kuhifadhisha Qurani Zanzibar.
Na Mary Julius
Jumla ya wanafunzi 26 kutoka vyuo mbalimbali vya Wilaya ya Kusini kiwemo Jambiani, Bwejuu, Paje, Muyuni, Makunduchi na Kizimkazi wameshiriki katika mashindano ya kuhifadhi Quran kwa wanafunzi wa madrasa ambapo mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake ni Halima Amour Juma kutoka Kizimkazi Dimbani na kwa wanaume ni Maftah Hussein Saleh kutoka Jambiani Kibigija.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Alhaj Ayoub Mohd Mahmoud amewasisitiza waumini na viongozi wa dini ya kiislam kulipa kipaumbele Suala la kihifadhi Qurani kwa watoto kwa lengo la jamii kuwa na vijana wenye madili mema
Alhaji Ayoub ametoa kauli hiyo katika msikiti wa skuli ya Sekondari Hasnuu Makame wakati akifungua Mashindano ya kihifadhi Qurani kwa wanafunzi wa madrasa kutoka katika Maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Kusini ikiwa ni muendelezo Wa maashimisho ya siku ya Kizimkazi .
Amesema Suala la watoto kuhifadhi Qurani ni jambo lenye faida kubwa kwani linamkurubisha mja na mola wake hivyo ni Vyema viongozi wa dini,wazazi na walimu kuona umuhim wa kuliendeleza ili kuwajengea watoto kiimani na dini yao Hali itayopelekea pia kusaidia kupunguza mmongonyoko wa maadili.
Kwa upande wao mjumbe wa kamati Kuu ya Jumuiya ya kuhifadhisha Qurani Zanzibar Sheh Saleh Ali na Amiri kanda ya Kizimkazi Sheh Hassan Omar Khamis wamesema kuendelezwa kwa matamasha ya Ramadhan na matamasha mengine yanayofungamana na masuala ya dini ya kiislam kutasaidia kukuza harakati za uislamu ndani ya mkoa huo.
Nao wanafunzi walioshiriki katika mashindano hayo wamewashukuru viongozi wa nchi , wadini na wa madrasa kwa kuandaa mashindano hayo na kuwataka wanafunzi wenzao kushiriki katika mashindano hayo ambayo yanaleta manufaa hapa duniani na kesho akhera.