Zenj FM

Mbunge wa Mahonda akabidhi mitungi 150 ya Gesi kwa Mama Lishe na Baba Lishe

19 August 2024, 2:31 pm

Mbunge wa jimbo la Mahonda Abdallah Ali Mwinyi,akikabidhi mitungi ya gesi kwa kikundi cha ujasiriamali cha Baba na Mamalishe kilichopo Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Na Mary Julius

Jumla ya vikundi vitano vimekabishiwa vifaa ikiwemo kikundi cha mama lishe na baba lishe, kikundi cha Kazi iendele , Madrasa ya matetema , Madrsa ya Mahonda na Mipira ya Maji na Tanki kwa shehiya ya Kilombero.

Mbunge  wa jimbo la Mahonda Abdallah Ali Mwinyi, amesema wajibu wa viongozi wa majimbo ni kuisaidia serikali katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na miradi ya maendeleo, ili kutatua changamoto za wananchi wake.

Mbunge Ameyasema hayo katika hafla ya ugawaji wa mitungi ya gesi 150  kwa mama lishe na baba lishe, vifaa vya maji kwa wananchi wa shehiya ya Kilombero, mabati kwa madrasa ya Matetema na Mahonda, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2020/2025, iliyofanyika huko Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema anatambuwa kuwa katika jimbo hilo kuna changamoto nyingi ambazo zinawakabili na serikali imekuwa ikijitahidi kufanya kila juhudi kukabiliana nazo na kuwaletea wananchi wake maendeleo ili kuona wananchi wake wanaishi katika mazingira bora.

Sauti ya Mbunge  wa jimbo la Mahonda Abdallah Ali Mwinyi,

Akizungumzia kundi la mama lishe na baba lishe alisema ni kundi ambalo linahitaji kupata usaidizi ili kuendesha shughuli zao za  kuendelea kujiajiri wenyewe.

Aidha amewataka kujikusanya na kujisajili huku ofisi yake ikitafuta na kubuni njia mbali mbali za kuhakikisha wanawapatia mikopo ili kupambana na tatizo la ajira nchini.

Sauti ya Mbunge  wa jimbo la Mahonda Abdallah Ali Mwinyi,

Kwa upande wake Katibu wa Jimbo hilo Simba Haji Mcha, ametoa shukurani zao kwa mbunge huyo kwa adhma yake ya kutoa msaada huo.

Amesema kitendo ambacho amekifanya ni mwendelezo wake katika kuhakikisha anatekeleza kwa vitendo ilani ya chama ambayo alikabidhiwa na kuja kuifanyia kazi.

Sauti ya Katibu wa Jimbo Mahonda Simba Haji Mcha,

Wakitoa shukrani zao mama lishe na baba lishe wameomba kupatiwa mafunzo ya matumizi ya majiko hayo ili kuepusha hasara.

Aidha wameomba kupatiwa  hati za usajili kwa vikundi vyao ili kuweza kujiendeleza na kuweza kupata mikopo kwa haraka.

Sauti ya baba lishe.