Tamasha la Kizimkazi lawafikia wavuvi wilaya ya Kusini Unguja
16 August 2024, 3:42 pm
Na Mary Julius.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Shaban Ali Othman amesema dhamira ya Serekali zote mbili nchini ni kuimarisha Sekta ya uchumi wa bluu na kuona wavuvi wanapata tija na pato la taifa linaongezeka .
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Shaban Ali Othman amesema serkali itaendelea kuchukua juhudi za kuielimisha jamii juu ya matumizi na utunzaji wa rasilimali za bahari ili ziweze kunufaisha vizazi vya sasa na vjavyo
Akizungumza huko Kizimkazi wakati akifungua mafunzo ya siku Tano kwa wavuvi kutoka Shehia mbali mbali za wilaya ya kusini juu ya namna Bora na salama ya Uhifadhi na uchakataji wa samaki na mazao mengine ya bahari kiwa ni miongoni mwa harakati za kuelekea katika madhimisho ya Tamasha la siku ya kizimkazi.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza kipato kwa wavuvi na pia kuondosha matatizo mbali mbali ikiwemo ya uvuvi Haram na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe Pamoja na serikali inayojitokeza mara kwa mara.
Nae Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu Tanzania Dk Immanuel sweke amesema serekali imeona kuna umuhimu mkubwa wa kuandaa mafunzo hayo kwa wavuvi wadogo wadogo kutokana na mchango wao mkubwa wa kuisaidia jamii katika kupata Chakula na pia kujiwezesha kiuchumi.
Nao wavuvi hao wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kufanya shughuli zao za uvuvi kwa uhakika na kuahidi kuisambaza elimu hiyo kwa wavuvi wengine.