Zenj FM

Kumbi za starehe chanzo kufeli wanafunzi Kusini Unguja

15 August 2024, 5:30 pm

Baadhi ya walimu wakuu wa Mkoa wa Kusini Unguja .

Na Mary Julius

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja amefanya kikao kilischowashirikisha walimu wa skuli zote za serikali na binafsi za Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa na lengo kuandaa mikakati ya kuimarisha ufaulu wa wanafunzi katika mkoa huo.  

Walimu wa serikali na binafsi Mkoa wa Kusini Unguja wametakiwa kutimiza wajibu wao vizuri ili wanafunzi waweze kupata matokeo mazuri.

Akizungumza na Walimu Wakuu wa Skuli za Kusini Unguja baada ya kusikiliza vikwazo vinavyowakabili walimu wa mkoa huo katika kufikia ufaulu mzuri wa wanafunzi, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amesema  sekta ya elimu ni eneo muhimu sana katika kuleta mustakbal mwema wa jamii, mkoa huo na taifa kwa ujumla hivyo ni vyema kuhakikisha wanasimamia ufaulu mzuri wa wanafunzi. 

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud.

Walimu wakuu wa skuli mbalimbali za mkoa wa Kusini Unguja wamesema ufaulu mdogo wa wanafunzi katika mkoa huo unasababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa  ushirikiano kati ya walimu, wazazi na wanafunzi, utoro na utayari mdogo wa wanafunzi katika kujifunza.

Sauti za walimu wakuu wa Skuli za M,koa wa Kusini Unguja.