Zenj FM

Jamii yashauriwa kufuga wanyama walio ndani ya uwezo wao

15 August 2024, 4:58 pm

Paka wanaofungwa.

Kila ifikapo Agosti 15 dunia inaadhimisha siku ya wanyama wasio na makazi.

Mkurugenzi wa Idara  ya Maendeleo na  Mifugo Asha Zahrani Mohd ameitaka jamii kushirikiana kwa pamoja ili kuwapatia chanjo mbwa na paka wanao zagaa mitaaani.

Akizungumza na Zenj FM ofisini kwake Maruhubi Mkurugenzi Asha amesema  chanjo watakayopatiwa wanyama hao itawakinga na maradhi ya kichaa cha mbwa ambacho huwaathiri wanyama na binadamu.

 Mkurugenzi amesema  kumekuwepo na ongezeko la wanyama wasio na maakazi hali hiyo  inasababishwa na jamii kufuga wanyama wengi  walio nje ya uwezo wao

Aidha ameitaka jamii kuwapeleka paka na mbwa katika idara ya mifugo  kwa lengo la kuwatoa vizazi ili kupunguza ongezeko la kuzaliana kwa wanyama hao.

Mkurugenzi Wa Idara  ya Maendeleo na  Mifugo Asha Zahrani Mohd.