Zenj FM

Mwakilishi wa jimbo la Malindi achangia ufaulu skuli ya Hamamni

9 August 2024, 7:03 pm

Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Hamamni akimkabidhi bahasha mwalimu wa skuli hiyo katika hafla ya kuwapongeza walimu hao wakiwa na Mwakilishi wa jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum (aliye vaa miwani)

Na Mary Julius

Katika matokeo ya kidato cha sita ya mwaka huu skuli hiyo imeweza kufaulisha kwa kupata daraja la kwanza wanafunzi 18, daraja na pili wanafunzi 94 kwa upande wa daraja la tatu wanafunzi 43 huku mwanafunzi mmoja akipata daraja la nne.

Mwakilishi wa jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum amepongeza walimu wa Skuli Ya Sekondari ya Hamamni , kwa kupata matokeo mazuri ya kidato cha sita ya mwaka 2024.

Mwakilishi ametoa pongezi hizo katika hafla fupi ya iliyoandaliwa na skuli  ili kuwapongeza walimu wa skuli ya hamamni iliyo ambatana na kupata chakula cha mchana kwa walimu na mwakilishi huyo katika ukumbi wa skuli

Amesema Matokeo hayo yamekuwa ni mwangaza kwa maendeleo ya elimu katika eneo hilo, na ni mfano mzuri wa mafanikio yaliyopatikana  kupitia bidii na kujitolea kwa walimu.

Aidha Mwakilishi amewahakikishia kutoa msaada wowote utakao hitajika ili kuboresha zaidi mazingira ya elimu katika jimbo hilo.

Sauti ya Mwakilishi wa jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum 

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Khamisi Hamad Khamis amesema lengo la hafla hiyo ni kupongezana na kufarijiana baada ya matokeo mazuri ya kidato cha sita ili kupeana moyo.

Aidha amempongeza kamati ya skuli na Mwakilishi wa Jimbo la Malindi kwa kuweza kuwasaidia katika kuhakikisha kambi iliyo wekwa kwa ajili ya maandalizi ya wanafunzi wanaojiandaa na  mitihani imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Sauti ya Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Khamisi Hamad Khamis

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Hamamni Duma Juma ameahidi kuendeleza ushirikiano na walimu ili kuhakikisha matokeo bora katika mitihani ijayo.

Suti ya Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Hamamni Duma Juma

Wakizungumza  kwa niaba ya walimu wenzake walimu wa skuli hiyo wameahidi  kuongeza juhudi za kufundisha ili kuhakikisha kwamba matokeo ya mwaka 2025 yanakuwa bora zaidi.  

Aidha walimu hao wamewaomba wazazi kusaidiana ili kuhakikisha watoto waote wanao jiandaa na mitihani wanakaa kambini.

Sauti ya walimu wa skuli ya Hamamni

Katika hafla hiyo walimu wamekabidhiwa bahasha yenye fedha taslim