Vikundi Zanzibar vya tahadharishwa mikopo ya riba
7 August 2024, 5:01 pm
Na Steven Msigaro.
Wanawake wajasiriamali wametakiwa kuacha kuchukua mikopo yenye riba kubwa na badala yake wachukua mikopo inayo tolewa na serikali.
Mkurugenzi Wa Idara Ya Maendeleo Jamii, Jinsia Na Watoto. Siti Abasi Ali ameahidi kusaidia vikundi vya wanawake wajasiriamali kuweza kupata mkopo isiyo na riba inayotolewa na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumza na wenyeviti, makatibu na washika fedha wa vikundi vya wilaya ya mjini huko seblen kwa wazee, mkurugenzi amesema mikopo yenye riba imekuwa kikwazo kikubwa kwa wajasiriamali katika kujikomboa kiuchumi hivyo kwa kuliona hilo serikali kwa kupitia fedha za uviko 19, halmashauri na manispaa kupitia uwezeshaji, imeweza kutoa mikopo isiyo na riba.
Aidha Mkurugenzi amevitaka vikundi visivyosajiliwa kupitia waratibu kuhakikisha vinasajiliwa kuepukana na changamoto za kukosa mikopo inayotolewa na Serikali.
Kwa upande wao wanavikundi wamesema mchakato mrefu wa upatikanaji wa mikopo ya serikali ndio unaosababisha wajasiriamali wengi kuachana na maombi ya mikopo hiyo na kuangukia kwenye mikopo yenye riba kubwa na kupata hasara.