Udongo sababu ya ucheleweshaji wa mradi wa ujenzi wa barabara Pemba
30 July 2024, 2:45 pm
Na Mary Julius.
Kampuni ya MECCO imetoa sababu za mradi wa ujenzi wa barabara ya chakechake/wete kuchelewa utekelezaji wake baada ya kubainika udongo wa barabara ya zamani unahitaji kuchimbwa na kuondolewa udongo kabla ya kuweka udongo mwingine na kusababisha ukubwa wa kazi kuongezeka.
Hayo yameelezwa na Muhandisi wa Kampuni hiyo Nassor Ramadhan wakati akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi huo kwa makamu wa pili wa rais alipokagua ujenzi wa mradi huo kisiwani Pemba.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amewataka wasimamizi wa mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi kwa vile barabara hiyo inaumuhimu mkubwa kiuchumi kwa wananchi kisiwani Pemba.
Naye Waziri wa Mawasiliano,Usaifirishaji na Uchukukuzi Dk Khalid Salum Muhamed amesema itakuwa vizuri mradi huo ukamilike kwa wakati ili kuzinduliwa januari mwakani.
Hata hivyo taarifa za ndani zinasema mradi huo umekuwa katika mazingira magumu baada ya mkandarasi kutolipwa kwa wakati malipo namba nne baada ya kuchelewa kwa siku 177 zaidi ya miezi sita na kulazimika kuchukua mkopo wa shilingi bilioni saba benki ili kuendeleza mradi huo.