Zenj FM

Maonesho ya wiki ya elimu ya juu ni fursa kwa wanafunzi Pemba

29 July 2024, 3:25 pm

Afisa Udahilishaji wa Taasisi hiyo Hija Adam Mtego akizungumza katika Maonyesho ya Wiki ya Elimu ya Juu Zanzibar yanayoendelea Gombani Chake Chake Pemba.Picha na Is- haka Mohammed.

Is- haka Mohammed.

Wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kisiwani Pemba wameombwa kutumia fursa za maonesho ya wiki ya elimu ya juu yanayoendelea visiwani hapa kwa ajili ya kuchagua vyuo na kozi wanazozipenda ili waweze kufanya maombi na kusajiliwa na vyuo hivyo.

Wito huo umetolewa na Mkuu Kitengo cha Mawasiliano na Masoko katika Taasisi hiyo Lilian Rugatika katika maonesho ya wiki ya elimu ya juu Zanzibar yanayoendelea Gombani Chake Chake Pemba.

Amesema wanafunzi na wananchi watakapotembelea maonesho  hayo watapata kujionea masuala mbalimbali yanayohusu masomo katika ngazi ya elimu ya juu.

Sauti ya Mkuu kitengo cha Mawasiliano na Masoko katika Taasisi hiyo Lilian Rugatika.

Naye Afisa Udahili wa taasisi hiyo Hija Adam Mtego amesema kupitia maonesho hayo wamekuwa wakitoa msaada wa maombi ya chuo kwa wanaohitaji kufanya maombi.

Sauti ya Afisa Udahilishaji wa Taasisi hiyo Hija Adam Mtego.

Baadhi ya wanafunzi wamepongeza hatua ya Taasisi Uhasibu Tanzania ya kufika kisiwani Pemba  kwenye maonesho hayo kwani ni fursa waliyoikosa kwa muda mrefu.

Sauti za wanafunzi.