Sera mpya ya utetezi, tumaini kwa wenye ulemavu Zanzibar
15 July 2024, 4:17 pm
Na Mary Julius.
Katika kikao hicho cha siku mbili wajumbe walijadili namna bora ya kutunga sera ya utetezi ya one advocacy one voice ambayo itasaidia jumuiya zote za watu wenye ulemavu.
Kukamilika kwa sera ya utetezi kwa taasisi za watu wenye ulemavu utasaidika katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapaza sauti zao kwa pamoja.
Akizungumza mara baada ya kikao cha siku mbili cha kujadili sera hiyo kilichoandaliwa na Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar na jumuiya zake 12 kilichofanyika katika ukumbi wa UWZ kikwajuni Unguja.
Mkufunzi Ally Saleh Amesema sera hiyo itawaongoza na kuwaelekeza namna ya kufanya utetezi ndani jumuiya za kimataifa kupitia serikali ya mapinduzi ya Zanzbar na itawezesha jumuiya za watu wenye ulemavu kuungana kwa pamoja na kushirikiana katika kufanya utetezi wa watu wenye ulemavu.
Kwa upande wake Meneja wa Nyumba ya Matumaini kutoka Jumuiya ya Umoja wa Watu wenye Vichwa Vikubwa na Mgongo Wazi Ruwayda Ramadhani amesema sera hiyo itakapokamilika itasaidia jumuiya hizo kushirikiana katika utetezi wa watu wenye ulemavu.
Aidha amewaomba wazazi kuto waficha watoto wanao zaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Nae Mjumbe wa Jumuiya ya Wakalimani wa Lugha ya Alama Zanzibar Zuhura Abeid Hemed ameiomba serikali kuajiri wakalimani wa lugha ya alama katika ofisi za umma, maskuli na hospital ilikuweza kuwasaidia watu wenye ulemavu wa kusikia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Masuala ya Ulemavu na Maendeleo Jumiishi Abdulkarim Abdalla Suleiman amesema sera itasaidia kufanya utetezi katika sekta mbalimbali ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao.