Zenj FM

Wilaya ya Kati wanufaika na ujenzi wa barabara

4 July 2024, 4:27 pm

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji (kati) akiwa Naibu Waziri wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Nadir Abdul-latif Yussuf pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Rashid Hadid katika ziara wilaya ya kati.

Na Kassim Adbi.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema kukamilika kwa miradi ya ujenzi wa barabara za Wilaya ya kati kumerahisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wakaazi wa maeneo zilipopita barabara hizo. 

Katibu Mkuu Dkt. Mngereza ameeleza hayo mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua barabara zilizokamilika kujengwa kwa Wilaya ya Kati.

Amesema Jumla ya kilomita 32.3 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na zimekua na tija kwa wakazi wa maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya hiyo.

Katibu Mkuu amesema kabla ya mradi huo kutekelezwa wananchi walikua wakipata shida kuyafikia maeneo muhimu kama vile sehemu za kilimo.

Sauti ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya kati Hassan Mrisho amesema uongozi wa Chama Wilaya ya kati umepata faraja kwa kiongozi huyo kushikiana nae pamoja katika ukaguzi wa barabara zilizojengwa ndani ya Wilaya ya kati

Aidha amesema, kazi iliofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ni kupigiwa mfano ambayo imewaridhisha wananchi wa Wilaya ya kati.

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya kati Hassan Mrisho.