Hatari, Zanzibar wanawake na vijana waathirika wa VVU
13 June 2024, 3:58 pm
Waziri wa Afya Zaznibar amesema baadhi ya tathmini za maambukizi mapya ya VVU zinaonyesha wanawake wameonekana na maambukizo mapya kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na wanaume, asilimia 3.0 ni wanawake na asilimia 0.7 ni wanaume.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imedhamiria kuendelea kupambana na maambukizi ya UKIMWI na kuzuia vifo vinavyotokana na maradhi mbali mbali ya kuambukiza yakiwemo UKIMWI, Homa ya Ini na Kaswende.
Akifungua mkutano wa uwasilishaji ripoti ya tathmini ya maambukizi mapya ya VVU kwa wadau mbali mbali Zanzibar Waziri Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara ya Afya kwa kupitia Kitengo Shirikishi UKIMWI, Homa ya Ini ,Kifua kikuu na Ukoma,kwa kushirikiana na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC) chini ya ufadhili wa CDC na usaidizi wa kitaalamu kutoka UCSF imefanikiwa kufanya tathmini hiyo ya maambukizi mapya ya VVU kwa mwaka 2024.
Amesema tathmini hiyo ni ya mara ya kwanza kufanyika hapa nchini na inaendelea kufanyika kwa Tanzania nzima na matokeo ya tathmini hiyo yatakuwa muendelezo wa nchi kujipima katika kufikia malengo ya dunia (SDG) ya kumaliza mambukizi mapya ya Ukimwi ifikapo mwaka 2030.
Akitoa muhtasari wa ripoti ya ufuatiliji wa maambukizi mapya ya VVU Meneja wa Kitengo Shirikishi Ukimwi Homa ya Ini kifua kikuu Dkt Mohamed Hassan Masoud amesema Zanzibar imeona umhimu wa kuanzisha muongozo wa ufuatiliaji wa maambukizi mapya kwa lengo la kutumia taarifa hizo kwa ufanisi.
Amesema takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa kati ya wateja 484 waliopimwa kunzia julai 2023 hadi mwezi mei 2024, 26 waligunduliwa kuwa na maambukizi mapya huku 258 wakiwa na maambukizi ya muda mrefu.
Nae mwakilishi kutoka CDC Dkt Nick Schhad amesema watahakiksha wanasimamaia vyema upatikanaji wa huduma sambamba na kufanya tafiti ambazo zitasaidia kutekeleza kazi kwa ufanisi hapo baadae.