Zenj FM

Damu haiuzwi Zanzibar

12 June 2024, 5:00 pm

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui.

Na Mary Julius.

Siku ya uchangiaji damu duniani huadhimishwa kila Ifikapo juni 14 kila mwaka,kwa hapa Zanzibar Maadhimisho haya yatafanyika katika ofisi za Mpango wa taifa wa damu salama sebleni.

Kuelekea siku ya uchangiaji damu duniani Waziri Wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amewataka Wananchi kutoa taarifa pale wanapotakiwa kutoa Pesa ili kwa lengo la kuuziwa damu katika hospitali Zote unguja na pemba kwani kufanya hivyo ni kosa Kisheria.

Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na waandishi Wa habari kuhusu siku ya wachangia damu duniani Amesema kuna taarifa za baadhi ya watendaji Hospitalini kuuza damu jambo ambalo ni kinyume na Utaratibu wa wizara.

Amesema kuwa hakuna kiwanda cha uzalishaji wa Damu hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kujitolea Kwa hiyari kuchangia damu ili kuokoa maisha ya Wahitaji wa damu.

Mazrui amesema kuwa mpango wa taifa wa damu Salama umejiwekea malengo ya kukusanya damu uniti 20 elfu kwa mwaka 2023-2024 na hadi kufiki mwezi March mwaka huu wamekusanya damu uniti kumi na Sita elfu mia moja hamsini na tano.

Sauti ya Waziri wa Afya Zanzibar.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mpango wa Taifa Damu Salama Ussi Bakar Mohd amesema mahitaji ya damu katika Hospitali yameongezeka kulinganisha na mahitaji ya Miaka ya nyuma.

Sauti ya AFisa Uhusiano Mpango wa Taifa Damu Salama Ussi Bakar Mohd