Mwakilishi atekeleza ilani kwa vitendo Chumbuni
3 June 2024, 5:41 pm
Na Mary Julius
Wakazi wa shehia mwembe makumbi kwa muda mrefu wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika shehia hiyo hali iliyo sababisha mwakilishi wa jimbo la chumbuni kuwachimbia kisima katika eneo lao.
Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji Khamis Kwanza amekabidhi tanki la maji lenye ujazo wa miilis 5000 pamoja na pampu na mipira kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Mwembe makumbi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo mwalikilishi amewaomba wakazi wa shehia hiyo kukitunza na kukilinda kisima hiicho pamoja na vifaa ili viweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Mwenyekiti wa Tawi la Mwembe makumbi b Bakari Mohammed Abdallah amesema kutokana na harakati za utengenezaji wa barabara katika shehia hiyo mabomba mengi ya maji yamekatwa na kusababisha ukosefu wa maji hivyio ujio wa kisima hicho kimekuwa mkombozi kwa wakazi wa eneo hilo
Aidha amempongeza Mwakilishi Miraji Kwanza kwa kuweza kutekeleza ombi hilo la kushimba kisima katika eneo hilo kwa haraka na kuahidi kukitunza pamoja na kulinda miundo mbinu ya kisima hicho.