Zenj FM

CCM Pemba yajipanga kushinda uchaguzi mkuu 2025

2 June 2024, 4:09 pm

Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Ali Issa Ali akimkabidhi kadi mwanachama mpya aliyejiunga na CCM akitokea ACT Wazalendo huko Mkoani Pemba.

Na Is-haka Mohammed. Pemba

Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Ali Issa Ali amewataka wazazi na walezi kuwalea vijana katika malezi bora ili kuwa na kizazi chenye maadili.

Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Ali Issa Ali ametoa wito kwa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi kuendelea kushirikiana katika ujenzi na uimarishaji wa Chama ili kiweze kufanya vizuri Zaidi.
Naibu katibu Mkuu huyo ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na wana CCM katika Wilaya ya Mkoani na Chake Chake akiwa katika ziara yake ya kujitambulisha kwa wanachama wa
kisiwani Pemba.

Ali amesema kufanya vizuri kwa chama hicho kunatokana na kuwepo kwa mashirikiano ya dhati kwa wananchi wa chama hicho hasa kupitia jumuiya zake ambazo ni za wazazi, wanawake na vijana.

Sauti ya Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Ali Issa Ali.

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba Seif Kassim Said amemweleza Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo mashirikiano waliyoanayo na Jumuiya nyengine
za Chama katika kufanya kazi ili malengo yaweze kufikiwa.

Sauti ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba Seif Kassim Said

Akitoa salamu za Mkoa wa Kusini Pemba Katibu wa Siasa, Itifaki, Uenezi na Mafunzo Mkoa huo Fat-hiya amesema chama mkoa huo kimaendelea na maandalizi mazuri kwa ajili ya kupata ushindi katika
uchaguzi mkuu ujao.

Sauti ya Katibu wa Siasa, Itifaki, Uenezi na Mafunzo Mkoa huo Fat-hiya.