Mwakilishi Chumbuni atimiza ahadi
31 May 2024, 4:21 pm
Na Mary Julius.
Shilingi milioni nane zinatarajia kutumika katika ujenzi wa mtaro wa maji machafu katika shahia ya Mwembe makumbi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi wa mtaro ambao umekatika na kusababisha mvua ikinyesha maji machafu kuingia katika nyumba za wakazi wa eneo hilo Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Miraji Khamis Kwanza amesema ujenzi wa mtaro huo utasaidia kuwaondolea wananchi wa eneo hilo changamoto walizokuwa wanakutana nazo hasa katika kipindi cha mvua.
Aidha wakilishi amewaomba wakazi waeneo hilo kutoa ushirikiano katika kuhakikisha mtaro huo unajengwa.
Kwa upande wao Wananchi wa shehia ya mwembe makumbi wamemshukuru mwakilishi wa jimbo la chumbuni kwa kuwaletea vifaa hivyo ambapo wamesema kupasuka kwa mtaro huo kumepelekea kipindi cha mvua maji kuingia katika nyumba zao na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hilo.
Aidha wananchi wamesema mtaro huo ambao juu upo wazi umekuwa ukihatarisha maisha ya watoto wadogo na watu wazima wanaoishi katika eneo hilo.