Bilion tisa zinatarajia kusogeza huduma za kimahakama Pemba
28 May 2024, 5:24 pm
Ujenzi wa kituo Cha kituo Jumuishu Cha Utoaji haki Kisiwani Pemba unajengwa kwa mkopo nafuu kutoka benki ya dunia na unatarajiwa kugahrimu zaidi ya shilingi bilioni tisa hadi kukamilika kwake, huku mkandarasi akitakiwa kuukabidhi Feb. 23 mwakani.
Na Is-haka Mohammed.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla amesema kuimarika kwa miundombinu katika mahakama kutatanua wigo katika upatikanaji wa haki kwa wananchi nchini pamoja na urahisi wa kupata huduma na kupungaza gharama.
Jaji Mkuu ameyasema hayo katika hafla ya utilianaji saini mkataba wa ujenzi wa kituo jumuishi cha utoaji haki Pemba kati ya Mahakama Tanzania na Kampuni ya Ujenzi ya M/S Costruction Limited ya Mogogoro hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa ZRA Gombani Chake Chake Pemba.
Amesema ujenzi wa Kituo hicho ambacho kitajengwa huko Mfikiwa nje kidogo ya mji wa Chake Chake Jaji Mkuu ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dr. Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar kwa kuendelea kuziunga mkono mahakama nchini.
Akizungumza mara baada ya kuweka Saini hiyo mtendaji mkuu wa mahakama kuu ya Zanzibar Kai Bashiru Mbarouk amesema kituo hicho kitakuwa na mazingira Bora ya utendaji Kazi na kuwapunguzia shida wananchi wa kisiwa Cha Pemba kufuata huduma za kimahakama katika maeneo ya mbali.
Aidha Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel amesema ujenzi wa kituo hicho unatokana na mashirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Zanzibar katika kutoa fursa katika kupatikana huduma jumuishi nchini.
Naye Mkandarasi wa ujenzi huo kutoka kampuni ya M/s Deep Construction ya Morogoro Binda Singh Jabal amesema kwa mashiriano kati ya Mahakama, Wasimamizi wa Ujenzi na wananchi watahakikisha mradi huo unakamilika Kwa wakati.