Mvua yaathiri uzoaji taka Wilaya ya Magharib A
1 May 2024, 7:28 pm
Na Rahma na Suleiman
Mkusanyiko wa taka kwa muda mrefu wawaibua wakazi wa Bububu meli nane.
Wananchi wa Bububu meli nane wadi ya kihinani wilaya ya magharibi( A) mkoa wa mjini wameilalamikia Manispaa ya wilaya hiyo kuwepo kwa taka muda mrefu .
Wakizungumza na zenji fm wananchi hao wamesema kukithiri kwa taka hizo kunahatarisha maisha ya wakaazi na wapita njia wa eneo hilo,
Aidha wamesema mkusanyiko huo unapelekea maradhi ya mripuko hususani katika kipindi hichi cha mvua zinazoendelea kunyesha, wamaeiomba mamlaka husika kulitafutia ufumbuzi suala hilo
Diwani wa wadi ya kihinani Nyange Hajji amekili kuwepo kwa changamoto ya taka katika eneo hilo amewaomba wananchi wa bububu meli nane kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu wanachokipitia.
Akithibitisha kuwepo kwa changamoto hiyo Mkuu wa Idara Huduma za Jamii Mazingira na Mipango Miji Baraza la Manispaa Magharibi (A) Tatu Hussen Abdalla amesema changamoto kubwa ya kukaa taka hizo kwa muda mrefu ni mvua kubwa za elnino zinazoendelea kunyesha hapa nchini.