Zaidi ya wajawazito elfu mbili wafikiwa na M-MAMA Zanzibar
25 April 2024, 5:48 pm
Mary Julius.
Wananchi wametakiwa kushirikiana na wizara ya afya katika kuwahimiza wajawazito kuhudhuria kliniki mapema ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Waziri wa afya Nassor Ahmed Mazrui ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kikao kazi cha kujadili mpango wa kuendeleza M-MAMA Zanzibar uliowashirikisha Wataalamu na wadau mbalimbali ambapo amesema kuwa Vifo vingi vya mama na mtoto vinatokana na baadhi ya
Kinamama kutohudhuria klinik na hospitali wakati wa Kujifungua hali inayosababisha matatizo ikiwemo kifo.
Mwenyekiti wa kikosi kazi cha M-MAMA Zanzibar Mohamed Habib amesema mpango huo unalengo la kuhakikisha vifo Vya mama na mtoto vinapungua iwapo utatumika vizuri.
Rahma Bajuni ni msimamizi wa mpango wa M- MAMA kitaifa Kutoka vodafone amesema ni wajibu wa kila mwanafamilia Kuhakikisha anatumia mpango huo ili kumuwahisha mama Na mtoto kuokoa maisha yao.
Disemba 2022 Zanzibar ilianza rasmi kutumia mpango wa M-MAMA na hadi kufikia 2024 zaidi ya mama na watoto elfu Mbili walisafirishwa kupitia mpango huo.