Uzio sababu ya utoro skuli ya Mguteni
17 April 2024, 4:46 pm
Na Rahma Hassan.
Uongozi wa Skuli ya Mguteni shahia ya Mbuyu Mtende wilaya ya Kaskazini wanaiomba serikali kulitafutia ufumbuzi suala la uzio katika skuli yao ili kuepusha kutoroka kwa wanafunzi hususani karibu na kipindi cha mitihani.
Wakizungumza na Zenji FM walimu wa skuli hiyo wanasema kutokuwepo kwa uzio kunapelekea wanafunzi tukoka muda wanaotaka pamoja na kuingia wanyama wakali kama mbwa ambapo kunahatarisha maisha ya wanafunzi na walimu.
Kwa upande wao wazazi na walezi wa wanafunzi wa skuli hio wamekiri kuwepo kwa suwala la utoro kwa wanafuzi na kujiingiza katika shuguli mbali mbaali ikiwemo vibarua pamoja na uvuvi jambo ambalo linapelekea kupoteza ndoto za wanafunzi.
Naye sheha wa Mbuyu Mtende ambaye pia ni mwenyekiti wa skuli hiyo Mkali Haji Jabu amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na hatua mbalimbali alizozichukua pia ameiomba serikali na taasisi mbalimbali kulitafutia ufumbuzi suala hilo.