Mrajis Zanzibar awakumbusha SHIJUWAZA kuchagua viongozi bora
15 April 2024, 4:37 pm
Na Mary Julius.
Shirikisho la Jumuiya za watu wenye ulemavu limesajiliwa rasmi mwaka 2014 mpaka sasa linawanachama 12.
Mrajisi Asasi za Kiraia Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla amewataka viongozi wa shirikisho la jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA) watakao chaguliwa kuziunganisha jumuiya zilizo chini yao.
Mrajisi ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi ulio fanyika katika ukumbi UWZ Kikwajuni Zanzibar amesema Kuna baadhi ya jumuiya zinajiona kuwa ni wakubwa kuliko shirikisho hilo hivyo ni wajibu wa viongozi watakao chaguliwa kuwaunganisha na kuwa kitukimoja ili kuleta maendeleo kwa wanajumuiya.
Aidha amewataka wapiga kura kuwachagua viongozi Bora watakao wavusha vyema kwa kipindi Cha miaka minne.
Akizungumza katika uchaguzi huo katibu mkuu wa zamani SHIJUWAZA Juma Salim Ali amesema shirikisho hilo katika kipindi Cha miaka nne limeweza kupata ufadhili wa sh billion 1 milioni 157 laki tano thelethini na tano elfu.
Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa Shirikisho la shijuwaza Ali Omary Makame aliyepita kwa kuchaguliwa kwa kura Za ndio kwa asilimia 89 amesema wamekusudia kujipanga na kuhakikisha wanasimamia haki na fursa za watu wenye ulemavu.
Walio chaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja na Mwenyekiti Mwanadawa Khamis Mohamme, Makamo Mwenyekiti ni Ali Omari Makame,Katibu Mkuu ni Tifly Mustafa Nahoda wengine ni Naibu Katibu kuu, Jide Khamis Swaleh,