Jamii yahimizwa kusaidia makundi maalum
13 March 2024, 5:04 pm
Jamii nchini imehimizwa kuutumia mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kukithirisha kufanya ibada kwa kusaidia mahitaji katika makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo elimu ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mapolo ya vyakula vyenye thamani ya zaidi ya shiling milioni nne kwa wanafunzi wa skuli ya Hasnuu Makame iliyopo Kibuteni, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa Mkoa wa Kusini Unguja Makama Ramadhan Mbanja amesema ameona umuhimu wa kutoa msaada huo katika skuli hiyo kutokana na kuwa ya bweni na ina wanafunzi wa makundi mbalimbali ikiwemo yatima, walemavu na wenye mazingira magumu hivyo utolewaji wa msaada huo utawapelekea wanafunzi hao kusoma masomo yao kwa uhakika.
Aidha mjumbe huyo amesema hatasita kutoa misaada kama hiyo katika skuli zingine na kwa jamii ili kuona kwamba wanafunzi wanaondokana na uhaba wa futari hasa katika kipindi hiki.
Mwalim Mkuu wa skuli hiyo Bakari Mohd Ali amezipongeza juhudi za mjumbe huyo kwa kujitoa kwake na kuona umuhimu kwa kusaidi skuli hiyo na kuahidi vyakula hivyo watavitumia kama ilivyokusudiwa.
Nao mwanafunzi wameshukuru Kwa msaada huo na kuomba taasisi na watu wenye uwezo kuiga mfano kama huo kwa lengo la kupata radhi za Allah pamoja na kukuza ustawi wa wanafunzi na elimu kwa ujumla.
Vyakula vilivyokabidhiwa ni pamoja na maharage gunia 5, unga wa ngano Pakti 7, sukari 4, tende, mchele, na mafuta ya kupikia box 4