Kaskazini A Unguja na Micheweni Pemba, kunufaika na Pharm Acces
4 February 2022, 5:05 pm
Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee na Watoto Nassor Ahmed Mazrui amesema wizara ya afya itaendelea kushirikiana na mashirika binafsi ili kuweza kuwasaidia wananchi wa visiwa vya Zanzibar.
Akizungumza katika makabidhiano ya kupokea vifaa vya kuboresha huduma za afya kwa mama wajawazito na watoto Waziri Mazrui amelipongeza shirika la Pharma Acces kwa kuuona uhitaji wa vifaa tiba katika Wilaya mbili ya Kaskazini Unguja na Micheweni Pemba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Phama Acces Tanzania Dk Kheri Marwa amesema Pharm Acces imejikita katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.
Shirika la Pharma Acces limetowa vifaa vyenye thamani ya million 92 kwa wizara ya afya ustawi wa jamii wazee na watoto kwa lengo la kuboresha huduma hizo.