Zenj FM
Madereva wa daladala watakiwa kutoingia na abiria sheli
24 November 2021, 1:26 pm
Na Thuwaiba Mohd: Afisa uhusiano wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nisharti Zanzibar ZURA Hassan Juma Amour amewataka wasimamizi wa vituo vya mafuta sheli kutoruhusu mtowa huduma kujaza mafuta kwenye gari ikiwa na abiria ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza.
Akizungumza na zenj fm katika ofisini za zura maisara mjini unguja afisa Hassan amesema kwa mujibu wa sheria za vituo vya mafuta ni kosa gari kujazwa mafuta ikiwa na abiria.
Nae muhasibu wa kituo cha kijangwani petrol station Abdallah rajab haji amesema ni vyema wahudumu wa sheli kutojaza mafuta kwa gari ambayo itakuwa na abiria.