Zenj FM
Wazanzibar watakiwa kuchanja chanjo ya uviko 19
16 November 2021, 2:06 pm
Na Thuwaiba Mohammed
Waziri wa afya ustawi wa jamii wazee jinsia na watoto Zanzibar Nasor Ahmed Mazrui amewataka wazanzibar kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya uviko 19 ili kujikinga na ugonjwa huo.
Waziri Mazrui ametowa wito huo na kusema wananchi wenye umri kwanzia miaka 18 na kuendelea kujihimu kuchanja kwani ukipata chanjo hiyo utakuwa umetengeneza kinga ya kupambana na ugonjwa huo na kuwakinga wengine.