Keifo FM

Kyela: Rupia ilivyomkosesha ubunge Ruhundwa

17 February 2026, 16:56

Pichani ni aliyekuwa mtia nia wa nafasi ya ubunge jimbo la Ngara na Mhariri Mkuu wa Jukwaa la Radio za Tamii Tanzania (Tadio) Hilali Ruhundwa. Picha na James Mwakyembe

“Sitarajii kurudi tena kwenye siasa, maana siasa ni uongo na ukweli”

Na James Mwakyembe

Aliyekuwa mtia nia wa nafasi ya ubunge jimbo la Ngara mkoani Kagera Hilali Ruhundwa katika uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 29 mwaka jana, amezungumza kwa mara ya kwanza na Keifo FM radio tangu kumwagwa na wajumbe kwenye uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Ruhundwa amesema fedha ilikuwa sababu kubwa ya yeye kuikosa nafasi hiyo ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika jimbo lake.

Kwa undani wa habari hii msikilize hapa chini akizungumza moja kwa moja kutoka Kyela mkoani Mbeya baada ya kumalizika kwa mafunzo ya ndani yanayoendeshwa na Tadio kwa radio wanachama, kwanza ameelezea kitu gani kilichomsukuma yeye kuingia kwenye kiny’ang’any’iro hicho.

Mahojiano na Hilali Ruhundwa