Keifo FM
Keifo FM
06/02/2026, 17:57

Katika tukio lisilo la kawaida wahitimu wa kujitegemea katika Shule ya Sekondari Keifo wameamua kununua keki na soda na kuwapelekea walimu kwa ajili ya kuwapongeza baada ya kuwawezesha kupata ufaulu mzuri katika masomo yao.
Na Emmanuel Jotham
Wahitimu wa kujitegema wali hitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Keifo iliyopo wilayani Kyela mkoani Mbeya wamewapongeza walimu wa shule hiyo kwa kuwasaidia wahitimu hao kufaualu masomo yao kwa kiwango cha juu.

Hatua hiyo ya kuwapongeza walimu wa shule hiyo imekuja baada ya wao kama wahitimu wa kujitegema yaan PC Kupewa ushirikiano wa hali ya juu pindi walipo kuwa shuleni hapo kwa miezi 9 na kuepeka wao kufaulu masomo yao.
Wakizungumza kwa furaha kubwa wahitimu hao wa kujitegemea wamesema wamemaua kununua cake na soda na kufurahi Pamoja na walimu hao kama alama ya ushindi katika safari yao ya elimu.
Awali akiwakaribisha katika tukio hilo la kupongezana mkuu wa shule ya sekondari keifo mwl skoti amesema kitendo walicho kifanya wahitimu hao kinaongeza motisha kubwa kwa walimu na kuwafanya waongeze bidi katika ufundishaji.
Kwa upande wao walimu wa shule ya sekondari keifo wamepongeza hatua ya wahitimu hao kwa kuwajali walimu walio wafundisha na kuwatakia kila rhahel kuelekea hatua inayo fuata katika safari ya elimu.
Shule ya Keifo sekondari ni shule ya binafsi inayo patika wilayani Kyela kata ya Serengeti ambayo inajumuisha wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita .
