Keifo FM

Kyela:Tusegelile wawafikia walemavu Kyela Msingi

30 July 2025, 17:17

Wanakikundi wa Tusegelile wakiwa na uongozi wa shule ya Msingi Kyela wakati walipotembelea na kutoa chakula kwaajiri ya watoto wenye uhitaji picha na James Mwakyembe

“tusiwafiche nyumbani watoto wenye ulemavu,wakifundishwa wanaweza kufanya kwa utimamu”

Na James Mwakyembe

Kikundi cha watu wa Rungwe waishio Kyela Tusegelile Group wametembelea na kutoa misaada ya kiutu kwa watoto wenye uhitaji maalumu katika shule ya msingi kyela, ili kuwafariji na kuwatia moyo watoto hao pamoja na walimu shuleni hapo.
Tukio hilo limefanyika leo katika shule ya msingi Kyela likiongozwa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Jackson Kajuni akiongozana na safu yake nzima ya viongozi wa kikundi hicho cha Tusegelile pamoja na walimu wa shule ya msingi Kyela.
Akizungumza wakati wa kutoa na kukabidhi misaada hiyo ya kiutu kwa uongozi wa shule ya msingi Kyela, Mwenyekiti wa kikundi hicho Jacksoni Kajuni amesema wameguswa kwa kuwa na wao ni sehemu ya wazazi wa watoto hao, hivyo kuwaomba wadau wengine kuungana nao katika jambo hilo.

Sauti ya mwenyekiti 11

Kwa upande wake Mwalimu Mshana ambaye ni Mwalimu wa darasa hilo la elimu maalumu, amesema darasa hilo lina watoto zaidi ya hamsini walio na mahitaji maalumu mbalimbali pamoja na kuiomba jamii kutowafungia watoto nyumbani, kwani watoto hao wakifundishwa wanafundishika.

Mwalimu kitengo 22

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya watoto na wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika shule ya msingi Kyela Lahel Mwabwagilo, amewashukuru wadau hao na kuwatakia kila lililo kheri katika harakati zao za kujipatia kipato.

Mtoto akishukuru 33
Picha ni wanakikundi wa Tusegelile wakiwa na walimu pamoja na wanafunzi wenye uhitaji malumu katika shule ya msingi kyela.

Mkami Maisangala ambaye ni Mwalimu mkuu msaidi katika shule ya Msingi Kyela amesema

Sauti ya Mkuu mdaidizi 44

Utoaji wa misaada hiyo ya kiutu kwa watoto wenye mahitaji maalumu unafanyika katika kipindi ambacho serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na wadau mbalimbali wakiwekeza nguvu kubwa katika kuijenga jamii iliyo na usawa.