Keifo FM
Keifo FM
20 June 2025, 17:19

Jumla ya shilingi milioni moja na laki tatu zimekabidhiwa kwa uongozi wa jumuiya ya vijana wilaya ya kyela kwa ajiri ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa jumuiya hiyo.
Na James Mwakyembe
Siku moja baada ya mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kiwanda cha Covenant Edible Oil Babylon Mwakyambile kuchangia fedha na mbao katika ujenzi wa nyumba ya katibu wa wazazi kyela hatimaye mdau huyo amerudi tena na kuchangia jumuiya ya vijana Ccm shilingi milioni moja na laki tatu pamoja saruji mifuko ishirini.
Mwakyambile ametoa mchango huo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya katibu wa jumuiya ya vijana Uvccm wilaya ya kyela iliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ikitanguliwa na kikao cha baraza kuu la vijana wilaya ya kyela.
Akikabidhi mchango huo kwa niaba ya Babylon Mwakyambile muwakilishi wa mdau huyo Frank Mwakapala amesema mchango huo umetolewa mahsusi kwa ajiri ya kuendeleza ujenzi ujenzi wa nyumba hiyo ambayo umeanza hivi karibuni.
Kuhusu muendelezo wa kuchangia Mwakapala amesema wataendelea kuchangia kwa kila hatua mpaka hapo ujenzi huo utakapokamilika na kuwapongeza jumuiya hiyo kwa kuanzisha mradi huo ambao amekiri kuwa alama itakayodumu vizazi na vizazi.

Akipokea cheti ya shukrani ya kutambua mchango wake katika shughuli za chama,Mwakapala ameshukuru na kusema wanatambua na kuupokea utambuzi huo kwa mikono yote.
Huu ni mwendelezo chanya wa mdau huyo kuendelea kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo kwa chama cha mapinduzi hapa wilayani kyela jambo ambalo limemfanya kuweka alama kubwa ya kukumbukwa na jamii ya wanakyela kwa vizazi vijavyo.