Keifo FM
Keifo FM
19 June 2025, 13:09

Jumla ya Mbao miamoja na arobaini zimekabidhiwa kwa jumuiya ya wazazi ili kukamilisha ujenzi wa nyumba ya katibu
Na James Mwakyembe
Hatimaye mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kiwanda cha mafuta ya kula Covenant Edible Oil Babylon Mwakyambile wake wa mbao miamoja na arobaini kwa jumuiya ya wazazi Ccm wilaya ya Kyela wenye thamani ya shilingi laki sita na elfu therathini.
Akipokea mchango huo kwa niaba ya katibu wa jumuiya ya wazazi Mary Rashid ambaye ni katibu wa Uwt wilaya ya Kyela amemshukuru mdau huyo na kumuomba kuendelea kuwaunga mkono katika kufanikisha ujenzi huo wa nyumba ya katibu wa Wazazi wilaya ya kyela.
Akizungumza baada ya kukabidhi nchango huo wa Mbao miamoja na arobaini mwakilishiwa wa mdau huyo wa maendeleo Frank Mwakapala amesema mbao hizo ni ahadi ya Babylon Mwakyambile aliyoitoa wakati wa harambee ndogo ya awamu ya tatu kuchangia ujenzi wa jengo la mtumishi wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Kyela.

Kadhalika Mwakapala amesema huo sio mwisho wa mdau na mkurugenzi huyo wa kuendelea kuunga mkono ujenzi huo,akibainisha kuwa yuko tayari mpaka jengo hilo litakapokamilika.
Kuhusu cheti cha utambuzi wa kuchangia alichopewa na jumuiya hiyo amesema Mwakyambile amefurahishwa sana na kuwashukuru viongozi hao kwa kutambua mchango wake katika ujenzi wa jumuiya mbalimbali za chama hicho kikongwe barani Afrika.
Babylon Mwakyambile ni kada wa chama cha mapinduzi na mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula cha Covenant Edible Oil kilichopo hapa wilayani kyela ambaye ameendelea kufanya mambo mbalimbali ya kichama ikiwemo kuchangia vifaa mbalimbali vya ujenzi wa ofisi za kata hapa wilayani kyela.