Keifo FM

Mwahula: Nilitoroka nyumbani miaka miwili

19 June 2025, 12:37

Pichani ni Siza Mwahula mlemavu wa viungo vya miguu tangu kuzaliwa kwake aliyefanikiwa kupitia ufundi wa cherehaniPicha na James Mwakyembe

Jamii wilayani Kyela imetakiwa kuacha tabia ya kuwafungia watoto wenye ulemavu ndani na kuwanyima haki zao za msingi.

Na James Mwakyembe

Kutana na Siza Mwahula mlemavu wa viungo ambaye anasimulia maisha yake jinsi alivyoondokana na utegemezi kwa familia na hata serikali kwa kutumia ujuzi wa ufunzi cherehani.

Licha ya kukiri kuwa wazazi wake hawakukubaliana na wazo lake la kuenda chuoni ili kujifunza ufundi.

Siza anasema ilimlazimu kutoroka nyumbani kupitia dirishani ili kuifuta ndota yake.

Fuatilia simulizi hii ili kujua undani zaidi