Keifo FM
Keifo FM
13 June 2025, 17:09

Jumuiya ya wazazi wilaya ya Kyela imetoa tamko la kumpongeza mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitishwa tena kugombea urais kwa awamu nyingine tena.
Na James Mwakyembe
Kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania jumuiya wazazi wilaya ya Kyela imetoa tamko la kumpangeza Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kulinda tunu za taifa zilizoachwa na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Tamko hili linakuja kufuatia kuwepo kwa baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni wanaharakati kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kuibuka na kuanza kumtusi Rais Samia na kubeza kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani.
Akisoma tamko hilo mbele ya mgeni rasmi wa kikao hicho ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge aliyewakilishwa na mwenyekiti wa Ccm wilaya ya Kyela Elias Mwanjala wakati wa kikao cha baraza kilichoambatana na harambee ndogo katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Kyela Richard Kilumbo amesema jumuiya hiyo inatambua kazi kubwa ya kuwaunganisha watanzania inayofanywa na Rais Samia.
Kilumbo akatoa ufafanuzi wa kwanini jumuiya hiyo imekuja na tamko hilo
Naye mbunge wa jimbo la kyela Ally Mlaghila amewapongeza wajumbe wa jumuiya hiyo na kuwataka kuwa makini kuchagua watu watakaojitokeza kuwania nafasi za Ubunge na udiwani huku akibainisha mambo yaliyofanyika katika kipindi chake.
Kwa upande wa Mjumbe wa mkutano mkuu Ccm taifa na mdau wa maendeleo Ramadhani Mwakitalu amepongeza viongozi wote wa jumuiya na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Kyela kwa namna wanavyokisimamia chama hicho huku na yeye akichangia mbao miamoja arobaini na tano zenye thamani ya zaidi ya shilingi laki sita.

Katika kikao hicho mbali na harambee pia kimetumika kutoa vyeti vya kutambua mchango wa wadau walioshiriki katika ujenzi wa nyumba ya katibu wa wazazi wilaya ya kyela ambapo kiasi cha shilingi milioni nane kimepatikana katika harambee jambo ambalo limefanya jumuiya hiyo kufikia lengo la bajeti yao ya shilingi milioni nane kwa awamu hii ya tatu.