Keifo FM

Kyela:Mwakyambile atunukiwa cheti wazazi ccm wakubali mziki

12 June 2025, 17:20

Pichani ni muwakilishi wa mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kiwanda cha kuzarisha mafuta cha Covenant Edible Oil kilichopo Kikusya wilayani kyela Frank Mwakapala Picha na James Mwakyembe

Mkugenzi wa kiwanda cha kuzarisha mafuta ya kula hapa wilayani kyela amechangia saruji na mbao katika ujenzi wa nyumba ya katibu wa wazazi wilaya ya Kyela.

Na James Mwakyembe

Mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kiwanda cha mafuta ya kula Covenant Edible Oil Babylon Mwakyambile ametunukiwa cheti cha mchangiaji bora kwa shughuli za maendeleo ndani ya chama cha mapinduzi ccm wilaya ya kyela.
Mbali na kutunukiwa cheti hicho Mwakyambile amechangia saruji mifuko kumi na tano yenye thamani ya shilingi laki tatu pamoja na mbao za kenchi zenye thamani ya shilingi laki sita katika ujenzi wa nyumba ya katibu wa jumuiya ya wazazi inayoendelea kujengwa hapa wilayani kyela.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi meneja wa kiwanda hicho cha Covenant Edible Oil Frank Mwakapala amewashukuru jumuiya hiyo kwa kutambua mchango wa mdau huyo huku akisema mkurugenzi huyo yuko bega kwa bega na jumuiya na chama katika kila hali.

sauti ya Frank Mwakapala kuhusu kukabidhi saruji

Pia Mwakapala amechangia na kukabidhi mbao zenye thamani ya shilingi laki sita zitakazochangia kukamilisha ujenzi wa nyumba ya katibu wa jumuiya hiyo konge katika chama cha mapinduzi hapa nchini tanzania.

Sauti ya Frank Mwakapala kukabidhi mbao

Pamoja na hayo Mwakyambile amewashika mkono wajumbe wa kikao hicho kwa kuwapatia kiasi cha shilingi laki nne ikiwa ni sehemu ya kupata maji wakati wa kikao salamu zilizopokelewa na mwenyekiti Elias Mwanjala ambaye amemhakikishia ushirikiano wa hali na mali mdau huyo.

Sauti ya Mwakapala kuhusu maji

Babylon Mwakyambile amekuwa mstari wa mbele kuchangia na kuunga mkono shughuli mbalimbali za chama cha amapinduzi wilaya ya kyela kuanzia ngazi ya chini ambapo katika nyakati tofauti tofauti amechangia na kufanikisha ujenzi wa ofisi nyingi za Ccm kata ikiwemo,Isaki,Itunge,Talatala na maeneo mengine hapa wilayani kyela.