Keifo FM

Kyela: Wafanya kazi wanao jitolea Tanesco wapewa zawadi

26 May 2025, 13:15

Picha mkuu wa wilaya na meneja wa tanesco wilaya ya kyela/picha na emmanul jotham

“Wafanya kazi walio pewa zawadi ni wale wa mkataba wa muda mfupi,ambao wamekuwaa na mchango mkubwa kwenye shirika katika kufanikisha ufanisi wake” meneja wa tanesco wilaya

Na Emmanuel Jotham

Shirika la umeme Tanesco  wilaya ya kyela limetoa zawadi mbalimbali kwa wafanya kazi wao bora kwa  mwaka 2024/2025 ikiwa ni katika kutambua mchango wao katika ufanisi wao wa kazi ndani ya shirika hilo.

Hafla hiyo ya kupongezana imafanyika hapa wilayani kyela huku  ikihudhuliwa na mkuu wa wilaya ya kyela  Josephine Manase katika kuhitimisha sherehe ya wafanya kazi mei mos ambayo kitaifa imefanyika mkoani singida.

Wakizungumza kwa furaha kubwa baadhi ya wafanya kazi wa shirika hilo la umeme tanesco wilaya ya kyela wamesema kuwa siri ya kuchaguliwa kuwa wafanyakazi bora ni kujituma na kujali kazi unayo pangiwa.

sauti ya wafanya kazi Tanesco

Akizungumza na mwandishi wa habari katika hafla hiyo afisa uhusiano wa tanesco wilaya ya kyela Alex Amry Amesema imekuwa ni utamaduni wa shirika hilo kutoa zawadi mbali mbali ili kutambua mchango wa wafanya kazi wao, katika kufanya kazi ambapo husaidia kuongeza hamasa ya kufanya kazi.

sauti ya afisa uhusiano Tanesco

Aidha meneja wa shirika la umeme  tanesco wilaya ya kyela Mhandisi Hasan Koko amesema lengo la kufanya sherehe hizo ni kuwaunganisha wafanya kazi pamoja na kuongeza chachu ya kufanya kazi kwa bidiii.

sauti ya meneja Tanesco wilaya ya kyela

Kwa upande wake  mgeni rasm katika sherehe hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya ya kyela Josephin Manase amelipongeza shirika la umeme wilaya ya kyela kwa kusambaza umeme vijijini kwa asilia kubwa hali inayo mfanya mkuu wa wilaya kujivunia shirika ndani ya wilaya ya kyela.

Hii imekuwa ni utamaduni wa mashirika mengi ya umma kutoa zawadi mbalimbali kwa wafanya  kazo wanao fanya kazi kwa bidii kupewa zawadi pindi zinapo fika sherere za mei mosi.

picha,mkuu wa wilaya ya kyela akikabidhi zawadi kwa mfanya kazi bora