

20 February 2025, 17:17
Wanachama wa chama cha mpainduzi ccm kyela mjini wilaya ya kyela wametembelea na kugawa misaada mbalimbali ya kiutu ili kuwakwamua kiuchumi wananchi wenye uhitaji maalumu katika kata hiyo.
Masoud Maulid
Ili kujenga jamii yenye ustawi sawa na bora Chama cha Mapinduzi Ccm kata ya kyela mjini kimetoa vitu mbalimbali kwa Kaya 15 zenye uhitaji kwa lengo la kuwafariji katika changamoto wanazopitia kipindi hiki.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kaimu Mwenyekiti wa Ccm ambae pia ni katibu wa chama hicho Yohana mwilongo amesema,dhamira ilikuwa ni kufanya zoezi la ugawaji wa msaada huo February 4 mwaka huu katika sherehe za kuzaliwa chama cha mapinduzi lakini wamelazimika kusogezwa mbele baada ya kuingiliana kwa ratiba.
Mwilongo ameongeza kuwa michango yote iliyofanikisha kununua vitu hivyo imetolewa na wanachama wenyewe wa ccm ambapo hawakuwa na mdhamini au mfadhiri yeyote ambapo wamefanikiwa kutimiza sehemu kubwa ya malengo yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Shabani Mwakapala amesema,kuna kaya nyingi zenye wahitaji na wameshindwa kuzifikia zote hivyo amewaasa Wanachama wengine kwenye maeneo yao kuwasaidia wenye uhitaji mbalimbali kwakuwa hawajapenda kuwa hivyo walivyo.
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika Barton Mwaseba amesema kuwa,msaada walioupokea ni mkubwa kwao na wameupokea kwa mikono miwili huku wakiwapongeza Wanachama wa Chama Mapinduzi kata ya kyela mjini kwa kuonesha moyo wa upendo kwa wahitaji.