

7 February 2025, 16:35
Serikali ya halmashauri ya wilaya ya Kyela imewapongeza wananchi kwa kuwezesha halmashauri kukusanya asilimia 98 za makusanyo kutoka katika vyanzo vyake.
Na James Mwakyembe
Baraza la madiwani la robo ya pili ya Mwaka la mrejesho kwa wananchi juu ya kipi kimefanyika limefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya kyela huku halmashauri ikivunja rekodi ya ukusanyaji mapato kwa kusanya jumla ya asilimia 98 ambayo haijawahi kutokea katika historia ya kyela.
Akifungua baraza hilo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kyela ambaye pia ni diwani wa kata ya Ikimba Katule Kingamkono amesema katika kipindi hicho serikali ya awamu ya sita imetoa fedha jumla ya shilingi bilioni moja nukta tano kwa ajiri ya kumalizia jengo la mama na mtoto katika hospitali ya wilaya ya Kyela.
Akitoa taarifa ya hali ya ukusanyaji wa mapato katika robo hii ya pili ya mwaka katule amesema halmashauri imeweza kukusanya mapato kwa silimia 98 katika robo ya pili jambo ambalo amekiri kuwa halijawahi kutokea katika wilaya ya kyela pamoja kuwashukuru mkurugenzi na watalaamu wote pamoja na wananchi kwa kutambua umuhimu wa kutoa kodi.
Pia Katule amezungumzia hali ya nidhamu kazini huku akibainisha kuwa jumla wa watendaji wawili wamefukuzwa kazi pamoja na kumshusha kiwango cha mshahara mtumishi mmoja baada ya kubainika kuwa na makosa ya kiutendaji kazini.
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya kyela limeketi ikiwa ni utaratibu ulijiwekea kwaajiri ya kutoa mrejesho wa taarifa mbalimbali kwa wananchi wake juu ya namna mambo mbalimbali ya kimaendeleo yanavyotekelezwa na viongozi waliowapa dhamana ya kuwaongoza katika kata zao.