

4 February 2025, 19:17
Mamia ya wananchi wamejitokeza katika viwanja vya mahakama ya wilaya ya kyela kusikiliza na kuwasilisha kero zao zilizotatuliwa na jopo la watalaamu wa sheria katika kilele cha wiki ya sheria hapa wilayani kyela.
Na Nsangatii Mwakipesile
Hatimaye kilele cha wiki ya sheria hapa wilayani kyela kimefanyika leo huku mkuu wa wilaya ya kyela Josphin Manase akiwapongeza viongozi na wafanyakazi wa Mahakama kwa kazi kubwa ya kushughulikia ipasavyo malalamiko ya wananchi na kuwasii kuendelea kutenda haki kwa muujibu wa sheria.
Akizungumza mbele ya wafanyakazi na wananchi walio jitokeza kwenye sherehe hizo Manase amewapongeza wafanyakazi kwa kupunguza msongamano wa kesi nyingi Mahakamani tofauti nah apo awali hivyo kuwaomba kuendelea kusimamia haki kikamilifu kwa kufuata misingi ya taaluma yao.
Katika hatua nyingine Manase amesema ni vema mahakama ikaon umuhimu wa kupeleka huduma za kisheria kwa wananchi kwenye kata zao ili kuwasogeza elimu Pamoja na kuwatatulia migogoro ihusuyo sheria katika maeneo yao.
Nae Hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kyela Andrew Severin Njau amewashukuru wadau na wananchi wote walioshiriki kwenye maadhimisho hayo na kuahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolwa na mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya kyela.
Madhimisho haya ya wiki ya sheria hufanyika kila mwaka ikiwa ni sehemu ya utambulisho wa shughuli mpya za mwaka wa mahakama ambazo hutanguliwa kwa kutoa elimu ambapo wadau wa sheria huzunguka katika kada mbalimbali kutoa elimu ihusuyo sheria hapa nchini.