Keifo FM

Busokelo:Rushwa marufuku uchaguzi serikali za mitaa

20 November 2024, 19:10

Mjumbe wa timu ya uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Busokelo Lewis Ally Mwasekaga akiwa katika studio za Keifo Fm Kyela kutoa elimu ya mpiga kura wa Novemba 27 picha na James Mwakyembe

Watanzania wametakiwa kijitokeza kuenda kupiga kura siku ya tarehe 27 Novemba katika zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika nchi nzima mwaka huu wa 2024.

Na James Mwakyembe

Wakati taifa la Tanzania likieleka katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu wananchi katika halmashauri ya wilayani Busokelo wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuenda kuchagua viongozi watakaowaongoza katika vijiji au mitaa yao.

Kauli hii inakuja wakati ambapo zoezi la kampeni za vyama vya siasa zimezinduliwa rasmi leo katika maeneo mbalimbali hapa nchini hii ikitoa fursa ya wagombea walioteuliwa na kupitishwa na vyama vya siasa kunadi sera zao mbele ya wananchi ili waweze kuwachagua.

Akizungumza na Keifo Fm mjumbe wa timu ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambaye pia ni afisa utamaduni sanaa na michezo halmashauri ya wilaya ya Busokelo Lewis Mwasekaga amewataka wananchi wote waliokidhi vigezo vya kupiga kura kujitokeza siku hiyo ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa maendeleo katika vijiji au mitaa yao.

Sauti ya Lewisi kuhusu watu kujitokeza kwa wingi 11

Akibainisha sifa za wapiga kura Mwasekaga amesema moja ya sifa zinazotazamwa zaidi ni kuwa sehemu ya waliojiandikisha katika daftari la mkazi zoezi lililoendeshwa kote nchini siku chache zilizopita hivyo kuendelea kusisitiza juu ya sifa hizo zitakazompa uhalali wa kupiga kura katika kijiji aua mtaa husika.

Lewisi sifa za kuchagua kiongozi 22

Naye Peter Tungu ambaye pia ni mjumbe wa timu ya uchaguzi wa serikali za mitaa na kaimu afisa habari wa halmashauri ya Busokelo amebainisha kuwa kampeni hizo zilizozinduliwa leo zitakwenda kwa muda wa siku saba pamoja na kuwaasa wananchi kutojihusisha na masuala ya rushwa kutoka kwa wagombea wanaotaka nafasi hizo.

Sauti Peter Tungu kuhusu muda wa kampeni 33

Kuhusu wajibu wa vyama vya siasa Tungu amesema vyama vyote vinapaswa kuzingatia miongozo yote waliyoipeleka kwa msimamizi wa uchaguzi pamoja na kuendesha mikutano ya kampeni pasna kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Sauti ya Tungu kuhusu wajibu wa vyama vya sisasa 44

Uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika Novemba 27 kote nchini Tanzania ambapo wananchi watatumia fursa hiyo kuchagua viongozi watakaowaongoza kwa kipindi kingine cha mika mitano.