Kyela:Wananchi jitokezeni kujiandisha daftari la mkazi
Keifo FM

Wananchi Kyela jitokezeni kujiandisha daftari la mkazi

30 September 2024, 16:56

Pichani ni Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Antukene Rashidi akiwa ofisini kwake picha na Nsangatii Mwakipesile

Wito umetolewa kwa wananchi wilayani hapa kujitokeza kujiandisha katika daftari la mkazi linalotajiwa kuanza mwezi ujao wa octoba.

Na Jamila Mwambande

Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji Afisa uchaguzi wa halmashauri ya wilaya ya kyela, Antukene Rashidi, amewataka wananchi kujitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la mkazi linaotarajiwa kufanyika mwezi octoba mwaka huu.

Haya yanajiri ikiwa zimesaria siku chache za kuanza kwa zoezi hilo ambalo tayari limekwisha kuanza kutekelezwa katika mikoa mbalimbali ya hapa nchini Tanzania kwa kutolewa mafunzo ya jinsi ya kutumia vifaa vya uandikishaji.

Akizungumza na keifo fm redio Rashid amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujindakisha kwenye daftari la mkazi ambalo litakuwepo kila kitongoji ambapo amebainisha kuwa zoezi hilo litaanza rasmi tarehe kumi na moja mwezi wa  kumi na litatamatika tarehe 20 mwezi wa huohuo wa kumi.

Sauti ya Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Kyela kuhusu kujiandikisha

Kuhusu sifa za mtua anayepaswa kujiandikisha kwenye daftarai hilo la mkazi Rashid amesema mtanzania yoyote mwenye akili timamu na mwenye umri wa miaka kumi na nane na kuendelea na awe mkazi wa eneo husika.

Sauti ya Atunkene afisa uchaguzi wilaya ya kyela kuhusu mtu mwenye sifa za kujiandikisha na kupiga kura

Kwa upande wa watiania wanaotaraijia kugombea nafasi za uongozi wa serikali za vijiji na mitaa ni lazima awe anajua kusoma na kwandika lugha ya Kiswahili na Kiingereza na awe na umri wa kuanzia miaka 21 na mgombea awe amedhaminiwa na chama husika.

sauti ya afisa uchaguzi kuhusu mtu anayepaswa kugombea nafasi ya uongozi

Uchaguzi wa serikali za mitaa,vitongojii na vijiji hunafanyika kila baada ya miaka mitano hapa nchini ikitoa nafasi ya wananchi kufanya machaguo mengine ili kutekeleza suala zima la demokrasia.