‘Wananchi’ wawafikia wazee Kyela
20 August 2024, 20:53
Uongozi wa timu ya Yanga Afrika umezuru wilayani Kyela na kuunda kamati ya timu hiyo katika masuala mbalimbali ya timu.
Na James Mwakyembe
Mratibu wa Yanga mkoa wa Mbeya Said Kastela amekutana na wazee wa Yanga wilayani Kyela kwa lengo la kuchagua kamati ya wazee itakayosaidia kusimamia mipango na maendeleo ya timu hiyo.
Uchaguzi huo umefanyika hapa wilayani Kyela ukihusisha mratibu huyo pamoja na wanachama wa timu ya Yanga wilaya ya Kyela.
Katika uchaguzi huo wamefanikiwa kuchagua nafasi tatu za uongozi zitakazoenda kusimamia mambo mbalimbali yatakayoazimiwa na timu.
Waliochaguliwa kwa nafasi ya Mwenyekiti imechukuliwa na Chief Kenedy Koloso huku makamu mwenyekiti ikikaliwa na Juma Ally Musira na nafasi ya katibu ikikaliwa na Michael Omary.
Pia katika kikao hicho kimeudhuriwa na machifu wa mkoa wa mbeya akiwemo Lwasi Ndemba Mwasile,Prince Mwahijo, na Kened koloso ambao uwepo wao katika uchaguzi huo ndio uliopelekea mafanikio ya tukio hilo la kuwapata viongozi watakaoenda kusimamia mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya timu ndani ya wilaya ya kyela.
Kufanyika kwa uchaguzi huo ni kielelezo cha uwepo wa demokrasia miongoni mwa wanachama wa timu hiyo huku lengo likiwa ni kuiona timu inatoka hatua moja kwenda hatua nyingine kisoka.