Keifo FM

Hersi Said, mashabiki kusherehekea ubingwa wa 30 Kyela

1 July 2024, 18:15

Pichani ni mratibu wa matawi ya Yanga wilaya ya Kyela Ayoub Kashiririka akitoa taarifa mbele ya keifo fm picha na James Mwakyembe

Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said anatarajiwa kuungana na mashabiki wa timu hiyo hapa wilayani Kyela katika sherehe za kuipongeza timu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa 30 msimu huu.

Na James Mwakyembe

Baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu (NBC Premier League) pamoja na Kombe la Shirikisho (CRDB Federation Cup) mashabiki na wanachama wa timu ya Young Africans hapa wilayani Kyela wanatarajia kufanya sherehe kubwa za kuipongeza timu yao kwa mafanikio makubwa waliyoyapata msimu huu.

Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika Julai 6 mwaka huu katika fukwe za Matema hapa wilayani Kyela ikiwaunganisha wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutoka mikoa saba ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe na Katavi ambapo wanachama na mashabiki watapata nafasi ya kufahamiana.

Akizungumza na kituo hiki mratibu wa Yanga wilaya ya Kyela Ayubu Kashiririka amesema mbali na kusherehekea ubingwa wao timu hiyo itafanya mambo mbalimbali ya kijamii kama mashabiki wa timu hiyo kuchangia damu salama pamoja na kuendelea kusajili matawi ambapo mpaka kufikia tarehe hiyo watakuwa wamesajili wanachama takribani mia tano hapa wilayani Kyela.

Sauti ya Kashiririka kuhusu sherehe hizo pamoja na kazi zinazotaraijwa kufanyika siku hiyo.

Pia Kashiririka amesema katika sherehe hizo wanatarajia kuwa na mgeni rasmi raisi wa timu hiyo Injinia Hersi Said ambaye mpaka sasa amethibitisha uwepo wake ambapo mashabiki pia watapata nafasi ya kuyaona makombe yao waliyoshinda katika msimu huu.

Sauti ya kashiririka kuhusu mgeni rasmi wa shughuli hizo

Kuhusu usajili wa mchezaji wa kiungo kutoka Simba Clatus Chama amepongeza ujio wa mchezaji huyo huku kisema msimu ujao utakuwa ni msimu wa majuto kwa watani wao pamoja na mashindano ya kimataifa huku akitamba kuwa msimu ujao lazima watinge fainali.

Sauti ya Kashiririka kuhusu ujio wa Chama katika kikosi hicho msimu ujao.

Klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wake wa 30 katika ligi kuu nchini Tanzania, ubingwa unaoifanya timu hiyo kuzidi kujikita zaidi kileleni kwa kuwa na vikombe vingi zaidi ya timu zingine tangu kuanzishwa kwa ligi hiyo.