Keifo FM

Mwakitalu apasua Nyasa kuwafuata vijana kambini Ikombe

19 June 2024, 15:44

Pichani ni Ramadhani Mwakitalu mjumbe wa mkutano mkuu CCM taifa akiwa na katibu mwenezi wilaya ya Kyela ndugu Emmanuely Mwamlinge Pamoja na Mgeni rasmi katibu wa itikadi enezi na mafunzo mkoa wa Mbeya Christopher Uhagile Picha na James Mwakyembe

“Vijana jitokezeni kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa chama kiko tayari kuwaunga mkono”Ramadhan Mwakitalu.

James Mwakyembe

Wakati kambi ya umoja wa vijana ikiendelea kupamba moto huko Ikombe hapa wilayani kyela mjumbe wa mkutano mkuu CCM taifa  Ramadhan Mwakitalu ametembelea kambi hiyo na kutoa fedha taslimu shilingi laki tano kwa viongozi wa jumuiya hiyo ili kuunga mkono kambi hiyo.

Msafara huo umeongozwa na mgeni rasmi katibu wa itikadi enezi na mafunzo mkoa wa Mbeya Christopher Uhagile pamoja na Emmanuely Mwamlinge ambaye ni katibu itikadi uenezi na mafunzo wilaya ya kyela pamoja na wajumbe wengine kutoka wilayani kyela.

Akizungumza katika viunga vya kambi hiyo Mwakitalu amewapongeza vijana wote waliojitolea muda wao kushiriki kambi hiyo maalumu kwa chama cha mapinduzi pamoja na kuwapongeza wadau mbalimbali walijitokeza kuunga mkono agizo hilo la chama wilaya,mkoa na taifa.

Sauti ya mwakitalu ya kuwapongeza vijana na wadau waliojitokeza kwenye kambi hiyo 111

Ameongeza kwa kuwataka vijana wote hapa wilayani kyela kuhakikisha wanajitokeza kugombea na kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu pamoja na kukabidhi kiasi hcho cha fedha shilingi laki tano.

Sauti ya Mwakitalu kuhuau kukabidhi fedha taslimu laki tano kwa uongzi 222

Akimakaribisha mgeni rasmi katika kambi hiyo katibu mwenezi wilaya ya Kyela Emmanuely Mwamlinge ametoa pongezi zake kwa mwenyekiti na katibu wa chama hicho kwa busara zao na moyo walionesha katika kulifanikisha jambo hilo pamoja na kuwataka vijana hao kugombea katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.

Sauti ya mwamlinge pongezi kwa mwenyekiti Elias Mwanjala na katibu wake 11
Ndug Ramadhan Mwakitalu mjumbe wa mkutano kuu taifa akiwa na viongozi wa chama cha mapinduzi Ccm Emmanuely Kiketelo Mwamlinge na katibu wa itikadi enezi na mafunzo mkoa wa Mbeya Christopher Uhagile

Kwa upande wake mgeni rasmi katibu mwenezi wa mkoa wa Mbeya Christopher Uhagile yeye amempongeza Ramadhan Mwakitalu pamoja wadau wote waliunga mkono kambi hiyo ambapo ametumia muda huo kuendelea kuwaomba kuendelea kujitolea kuchangia chao.

Sauti ya mgeni rasmi kuhusu pongezi zake kwa chama na wadau waliojitokeza kufadhiri kambi hiyo ya vijana

Akitoa neno kwa niaba ya vijana katibu ya jumuiya hiyo wilaya ya Kyela Peter Tungulu amemshukuru Mwakitalu kwa kuitikia wito wao na kubainisha kuwa kambi hiyo inajumla ya vijana mia moja hamsini katika ya mianne waliokuwa wametarajia kuwa nao katika vikao vyao na kusema idadi hiyo imeonesha kufanikiwa pakubwa.