Keifo FM

Wengine 9 waikacha CHADEMA Kyela

4 June 2024, 17:11

Pichani ni jengo la chama cha demokrasia na Maendeleo chadema wilaya ya Kyela Picha kutoka chumba cha habari

Wimbi la wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema kukihama chama hicho hapa wilayani kyela limeendelea kushika kasi baada ya wananchama wake wengine tisa kujinga Ccm.

Na Aidan Mwasampeta

Siku chache baada ya wanachama wa Demokrasia na Maendeleo kutimka na kujiunga na chama tawala chama hicho kimeendelea kupata pigo baada ya wanachama wake wengine tisa kutimkia chama cha  mapinduzi ccm hapa wilayani kyela.

Haya yanajiri ikiwa ni juma moja tangu wananchama wengine zaidi ya sita kujiunga na chama cha mapinduzi ccm akiwemo iliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji cha mpakani kilichoko ndandalo Benjamini Mwafyuma.

Wakizungumza wakati wakupokelewa na viongozi wa ccm kata ya Ndandalo wamesema kuwa wamejiunga na ccm kutokana na kazi kubwa inayofanywa na chama cha mapinduzi katika awamu hii ya sita chini Raisi Samia Suluhu Hasani kuwa imekuwa sababu kubwa ya kukihama chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini Tanzania.

………Voxpop ndandalo…

Kwa upande wake diwani wa kata ya Ndandalo Kefa Mwanganda akiwa sehemu ya viongozi wa kata walishiriki katika zoezi la kuwapokea wananchama hao wapya yeye amewapongeza wanachama hao wapya kwa uwamuzi wao wa kujiunga na ccm na kuwataka kuwa mabalozi wazuri kwa kuendelea kuzitangaza kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na ccm.

…………..Kefa…

Mgeni rasmi wa kuwapokea wanachama hao Emmanuely Kharison maarufu Bongo ambae ni mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Kyela amewataka wanachama hao kuwa wazalendo na chama na sio kuwa wazalendo wa watu hasa kwenye uchaguzi.

………….Bongo……

itakumbukwa kuwa juma moja lililopita mwenyekiti wa chadema wilaya ya Kyela Victoria Benson Swebe alikanusha juu ya kuwepo madai kuwa wanachama wake wanakihama chama hicho na kudai kuwa watu walionekana kuhama si wa chama hicho ni wanachama wa vyama vingine vya siasa ikiwemo NCCR Mageuzi.

Wanachama waliojiunga na ccma kutoka kata ya Ndandalo ni tisa ambao ni Baraka Mwamsiku,Angel Kajela,Sikujua Kalongo,Wilson Mwakamsale,Sarah Ndondwa,Tummenye Kalunduka,Helena Bakinge,Mwakisambwe pamoja na Emelita Kalenge.