Kyela:Harufu mbaya yatatiza afya za watu Butiama
31 May 2024, 18:25
Kutokana na hali ya mrundikano wa taka ulikithiri katika kizimba cha soko la jioni Kapwili wamelalamiki harufu mbaya inayosababishwa na kujaa kwa taka kizaimbani hapo.
Na Nsangatii Mwakipesile
Wananchi na wafanyabiashara katika soko la jioni la njia panda kapwili wameitaka mamlaka ya mji mdogo wa Kyela kukiondoa kizimba kilichojaa taka ili kurejesha hali ya amani sokoni hapo
Kauli hiyo inakuja kufuatia kadhia kubwa ya harufu mbaya katika eneo hilo ambayo imesababishwa na mrundikano wa taka ambazo hazijaondolewa kwa muda muafaka na mamlaka zinazohusika na uzoaji wa taka.
Akijibu kuhusu kadhia hiyo mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Kyela Emmanuely Kharison maarufu Bongo amesema kutokana na upungufu wa magari unaowakabili mamlaka ya mji mdogo ndiyo sababu iliyopelekea kushindwa kutoa taka hizo kwa muda muafaka.
Kadharika Bongo amewataka wananchi wa maeneo yote hapa wilaya ni kyela kuwa wavumilivu wakati huu serikali ikiendelea kulitafutia suluhu jambo hilo ambapo amesema hivi karibuni litatatuliwa.
Katika hatua nyingine Emmanuely Kharson amewataka wenyeviti wote wa mamlaka ya mji mdogo kuhikikisha wanawahamasisha wananchi wote wanaozungukwa na mifereji katika makazi yao kuhakikisha wanaisafisha na kuizibua ili kurejesha hali ya usafi wa mazingira.
Suala mrundikano wa taka katika vizimba hapa wilayani kyela limekuwa tatizo la muda mrefu ambalo limekuwa na panda shuka katika utekelezaji wake kutoka mamlaka ya mji mdogo wa kyela hali ambayo imekuwa ikizua gumzo kwa wananchi wanaozungukwa na vizimba hivyo.